Saturday 8 October 2011

SIASA, HAKI YA MWANANCHI

Tokea mashariki, magharibi hadi kazkazini,
Wananchi wao hoi, kakimbilia tu ugimbi,
Uhara ndani vichwani, mada ni bungeni,
Siasa ifanye kazi, haki ya mwananchi.

Wao uwanjani, wamejawa uhasidi,
Waliochini miongoni, wamtafuta halili,
Aje piganie maslahi, uja kuwaondokeni,
Siasa ifanye kazi, haki ya mwananchi.



Bwana na bibi, wote ukosefu ujaji,
Watoto pia shuleni, masomo katupila mbali,
Kwani shibe hii, i wapi jameni,
Siasa ifanye kazi, haki ya mwananchi.


Bungeni sasa hivi,honga ni kuhonge,
Vigumu kuzua siri, nani mwenyewe aje,
Mwaminifu kwa nchi, kaje siasani kajitolee,
Siasa ifanye kazi, haki ya mwananchi.


Basi kwa kimoja, imani kati ikiongoza,
Mlango tushafika, kamwe sote hatutozusha,
Yote yale madaraka, yenu ya kuhonga,
Siasa ifanye kazi, haki ya mwananchi.


Bila ya hongo, tumaini kwa amani,
Heshima kibao, waheshimiwa na wananchi,
Tuungane mwanzo, tamati tushikaneni,
Siasa ifanye kazi, haki ya mwananchi.

1 comment:

Anonymous said...

kiswahili sanifu...the flow is is cool and message is deep.tho am not an expert..i do understand..peace ..ts michaelndetu .peace!