Saturday 5 November 2011

kuchanuka

Mitaani na miji, yote ina habari.
KIla mmoja gwiji, zaidi ya bahari.
Yamekuwa theluji, maisha kifahari.
Mkubwa kazi siji, mshahara tayari.
Sifaulu kwa aji, mwenyewe nimekiri.
Tumewacha vipaji, sawa tujihadhari.
Kweli hamna taji, je, kuchanuka hakuleti faida?

Suruali ndefuzi, wamezifanya zao
Binti wa siku hizi, maringo kwao ngao.
Heshima makaazi, hubadilisha wao.
Kuolewa ni ngazi, Maanake mazao.
Huvaliaa wazi, nani kati yao.
Ndani yake mapenzi, yeshi bila mpango.
Kweli hamna vazi, je, kuchanuka hakuleti faida?


Wanaume vipuli,kamaa wasichana.
Sisemi afadhali, nywele hawajachana.
Wamezisonga keli,Muumba wayaona?
Kale maisha kali,hayakuonekana.
Chakula na mahali, ndivyo muhimu sana.
Kamwe sitokubali,nishafahamu kina.
Kweli hamna sali, je, kuchanuka hakuleti faida?


Macho yamefunguka, kuna zuri na baya.
Mwonye dada na kaka, akubali haaya.
Mwisho akishafika, tujionee haya.
Upya unakubalika,  matumizi mabaya.
Yasiyokubalika, wewe yatakufinya.
I imebadilika, haitaweza waya.
Kweli hamna paka, je, kuchanuka hakuleti faida?








bosco

No comments: