Monday 31 October 2011

JUA

Mapenzi nauliza swali, laniwasha moyoni ndani.
Chozi lanitoka la hisi, niwazapo nini mapenzi.
Kanipe jibu mimi nali, uondoke nipe nafasi.
Masikini hoi niishi, mapenzi nipate juaa.

Nao wakubwa huwaachi, wadogo mwako miguuni.
Marafiki hoja kundini, siri kugamba wazi penzi.
Hucheka na hulia na wengi, wakisimuli ni alhani.
Jicho langu kabisa wazi, mapenzi nipate juaa.

Ni furaha tele undani, matawi yake tamu kweli,
Tumulikie mwanga basi, ufunze dhahiri shairi.
Tusije tukenda kwikwikwi, kwako tufahamu hisani,
Utuandalie harusi, mapenzi nipate juaa.

Yepi wewe uje amini, nikishafunga huu beti.
Kizazi kipya u mnyimi, safari tu mali mbioni.
Aliye na asiye haki, hakosi kukutamani.
Niongoze vema hadi, mapenzi nipate juaa.


bosco