Saturday 29 October 2011

Kakuchagua

Moyoni nikikuonani, nahisi raha maishani.
Mawazo mengi uchunguni, yatoka kiwa karibuni.
Nguvu wewe kanitiani, Mwandani tangule zamani.
Linitia mizizi ndani, akili zangu zote nani.
Basi unizitunzieni, mwingine haiwezekani.
Kakuchagua wa imani, nibebee kama sahani.

Ulimi wako midomoni, najihisi huru mwilini.
U tofauti samahani, jiji zima lakutamani.
Nafasi nawapatieni, nyie tu maoni semeni.
Nabakia naye jirani, ndugu hayo yasikieni.
Hizo kele zatoka chini, nasi tukipaa angani.
Kakuchagua wa imani, nibebee kama sahani.

Nishike ewe mikononi, tipo kati ya msituni.
Wawinda wamo mawindoni, tusije tukenda motoni.
Penzio halitakikani, twaonwa adui machoni.
Ulinihaidi rohoni, hutonacha hata kuweni.
Mwenzio nakushukuruni, kwa kuniweka maanani.
Kakuchagua wa imani, nibebee kama sahani.




bosco

No comments: